The House of Favourite Newspapers

Polisi Wamkamata aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Yahaya Nawanda

0

Jeshi la polisi limemkamata aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Yahaya Nawanda (46) kwa tuhuma za kumwingilia kinyume na maumbile mwanafunzi wa chuo ambaye jina lake limehifadhiwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza leo, Juni 13, 2024 Naibu Kamishina wa Polisi na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, DCP Wilbrod Mutafungwa amesema mtuhumiwa huyo amekamatwa leo jijini Mwanza saa 6.00 mchana.

Kwa mjibu wa Kamanda Mutafungwa amesema tayari jeshi hilo limeanza kufanya mahojiano sanjari na kufanya uchunguzi wa kimaabara kuhusiana ana tuhuma hizo na baada ya kukamilisha uchunguzi utafikishwa kwenye ofisi za mashtaka.

Leave A Reply