Polisi Warushiana Risasi na Majambazi Waliovamia Sheli, Mmoja Auawa

JESHI la Polisi Mkoa wa Kagera limefanikiwa kuzuia tukio la ujambazi wa kutumia silaha lililokuwa linapangwa na majambazi watatu waliokuwa wanajaribu kuvamia kituo cha mafuta (petrol station) cha Benaco Oil kilichopo Benako Wilaya ya Ngara mkoani humo.

Kamanda Mkuu wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kagera William Mwampaghale amesema tukio ilo lilitokea tarehe 7/12/2022 majira ya saa 2:30 usiku katika kijiji cha Rwakalemela kata ya Kasuro wilaya humo,ambapo majambazi watatu walirushiana risasi na polisi majambazi wawili walikamatwa mmoja kati hao alifariki wakati akikimbizwa hospitalini uku jambazi mmoja akifanikiwa kutoroka.