Polisi Watapakaa Mwanza, Hivi Ndivyo Halio Ilivyo

JESHI la Polisi waliojihami kwa silaha za moto na mabomu ya machozi wamezingira na kufunga njia za kuingia na kutoka Tourist Hotel (zamani Tai Five) iliyopo Kitangiri Mwanza ambako Kongamano la Katiba Mpya lililoandaliwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) lilitarajiwa kufanyika leo Jumatano, Julai 21, 2021.

Polisi wamefunga Barabara ya Kona ya Bwiru – Kitangiri ambapo ndio njia ya kuelekea ukumbi wa hoteli hiyo. Kila anayepita njia hiyo uhojiwa kabla ya kuruhusiwa kupita au kuzuiwa kwa kutakiwa kupita njia nyingine. Magari matano ya polisi likiwemo la kubeba watuhumiwa na wafungwa maarufu kama karandinga yakiwa yameegeshwa nje na ndani ya uzio wa hoteli.

Wakati hayo yakitokea, viongozi wa Chadema akiwemo mwenyeki wao, Freeman Mbowe na wengine 10 wakiwemo, Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Serengeti, John Heche, Mwenyekiti Bavicha, John Pambalu na wengine wamekamatwa na Jeshi hilo usiku wa kuamkia leo, lakini polisi bado haijaeleza sababu ya kuwashikilia.

Alipotafutwa na Global Publishers kwa njia ya simu leo Julai 21, Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Ramadhani Ng’anzi kuhusu taarifa simu yake imeita mara kadhaa pasi na kupokelewa.


Toa comment