The House of Favourite Newspapers

Polisi Yafunguka Kisa cha Diwani Chadema Kukatwa Mapanga

KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Urich Matei amefunguka na kusema kuwa kifo cha Diwani wa Kata ya Nawala tarafa ya Ifakara wilayani Kilombero, Godfrey Joackim Luena (CHADEMA) aliyefariki kwa kupigwa mapanga huenda ni kisasi.

 

Matei amesema kuwa kiongozi huyo (Luena) kuna wakati aliwahi kuwaambia wanakijiji kuwa mtu ambaye alikuwa anafahamika kwa jina la Kenani Haule ndiye alikuwa anawasaliti hivyo baada ya muda mtu huyo aliuliwa kwa kupingwa mapanga.

 

“Mwanzoni mwa mwaka 2016 watu wa Nawawala walikuwa na ugomvi kati ya wanakijiji na bodi ya sukari, akiwa diwani wa eneo lile, Luena alisimamia wananchi wake kudai lile shamba. Kuna kesi ambayo ipo mahakamani mpaka sasa inaendelea lakini aliwaambia mtu mmoja anaitwa Kenani Haule ndiye tatizo.

 

“Luena aliwaambia kuwa huyo Kenani ndiye anawasaliti, hata kama Kenani akifariki basi wao watakuwa na uwezo wa kupata shamba, muda mfupi Kenani aliuawa kwa kukatwa mapanga tukio ambalo lilitokea kama lilivyotokea kwake.

“Kimsingi tunaamini Luena atakuwa ameuawa kwa ajili ya kisasi baada ya kifo cha Kenani Haule,” alisema Matei.

 

Aidha, Kamanda Matei alidai kuwa jeshi la polisi bado linaendelea na uchunguzi na msako mkali unaendelea na kudai hilo ni tukio baya kutokea Morogoro kwa sababu wamempoteza kiongozi wa wananchi wa Nawala na kuwataka wananchi ambao wana taarifa juu ya mazingira ya mauaji hayo watoe taarifa polisi ili waweze kuzifanyia kazi zaidi.

HAPA NDIPO ALIPOLALA AKWILINA AKWILINI- VIDEO

Comments are closed.