The House of Favourite Newspapers

Polisi Yakiri Kumpiga Risasi Raia Kwenye Maandamano ya Chadema

RPC Mambosasa.

 

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amekiri kuwa mtu mmoja alipigwa risasi na polisi kwa bahati mbaya wakati wakiwatawanya wafuasi wa Chadema walioandama jana Februari 16, 2018, jioni.

 

Wakiongozwa na mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe wafuasi hao waliandamana kuelekea ofisi ya msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Kinondoni, Aron Kagurumjuli ili kudai viapo vya mawakala kusimamia uchaguzi wa chama hicho.

 

Anayedaiwa kuuawa.

 

Aidha, ufafanuzi wa Mambosasa haukuweka wazi iwapo mtu huyo alipoteza maisha ama la. Inadaiwa kuwa aliyepigwa risasi na kupoteza maisha ni mwanafunzi wa elimu ya juu.

 

Maandamano hayo yalianzia viwanja vya Buibui Mwananyamala ulipokuwa ukifanyika mkutano wa kampeni wa Chadema, yalipofika Mkwajuni wafuasi hao walitawanywa na polisi, huku mtu mmoja aliyekuwa kwenye basi la daladala akidaiwa kupigwa risasi na kufariki dunia.

 

Mambosasa amesema “Walizuia mwendo kasi, wakaanza kupiga mawe kwa hiyo kati ya risasi za hewani zilizopigwa kuwatawanya kuna iliyompata (mtu).”

POLISI Yakiri Kumpiga Risasi Raia Kwenye Maandamano ya CHADEMA

Comments are closed.