The House of Favourite Newspapers

Polisi Yasema Kesi ya Dk Shika Haina Mashiko

Dk Louis Shika.

JESHI la Polisi Kanda Maalumu yaDar es Salaam, limesema kesi ya Dk Louis Shika hawataendelea nayo kwa kuwa nyumba tatu za mfanyabiashara maarufu Said Lugumi alizoahidi kuzinunua zote zipo na hazijapata mnunuzi.

 

Hayo yamesemwa leo Desemba 6, 2017 na Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar, Lazaro Mambosasa wakati akizungumza na wanahabari, amesema kesi ya Dkt. Shika haina mashiko hivyo hawataendelea nayo kwa kuwa nyumba hizo zipo na hajatia hasara yotote.

 

Mambosasa amesema Dk Shika alikuwa akitamba kuwa ana fedha kumbe uwezo wake ni mdogo na kusababisha  kushindwa kulipa asilimia 25 kwa kila nyumba hizo.

 

‘‘Dk Shika ni wa kumuonea huruma hana kitu, tulisema tunamchunguza na tutampeleka mahakamani lakini tumeona kesi yake haina mashiko ndiyo maana tumeamua tusiendelee nayo,” amesema Mambosasa.

 

Novemba 9, 2017 kampuni ya udalali ya Yono kwa niaba ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) iliendesha mnada wa hadhara wa nyumba mbili za Lugumi zilizoko Mbweni JKT na nyingine Upanga jijini Dar es Salaam ambazo zote Dk Shika alifikia bei ya kuzinunua kwa Tsh. Bilioni Sh 3.2.

 

Jeshi la polisi kanda hiyo lilimshikilia na kumwachia kwa dhamana Dk Shika ambaye alikuwa akituhumiwa kwa kuharibu mnada baada ya kushindwa kulipa asilimia 25 ya fedha hizo ambapo nyumba za Mbweni JKT alifika bei kwa Sh. 900 milioni na nyingine Sh 1.1 bilioni, huku ya Upanga alifika bei ya Sh 1.2 bilioni.

(Stori na Pamela Chilongola, Mwananchi)

KUBENEA: Sinunuliki CCM, Siwezi Kuhama CHADEMA Wala Kuisaliti UBUNGO

 

Comments are closed.