The House of Favourite Newspapers
gunners X

Polisi Yasitisha Wito kwa Lissu Yasema Aendelee na Kampeni

0

POLISI Kanda Maalum ya Dar es Salaam leo Ijumaa Oktoba 2, 2020, imesitisha wito wa kumtaka mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu,  kufika kituo cha polisi na badala yake aendelee na ratiba za kampeni za uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu.

Kwa mujibu ya barua iliyotumwa kwa Mwenyekiti wake wa Chama, Freeman Mbowe, Lissu anatakiwa kuripoti polisi leo 02/10/2020 kwa ajili ya mahojiano kufuatia kauli na matamshi yake ambayo amekuwa akiyatoa kwenye mikutano yake ya kampeni dhidi ya maafisa wa polisi huku akimtuhumu Lissu kugombana na wakuu wa polisi.

Leave A Reply