Polisi Yaua Majambazi Watatu Kigoma

JESHI la Polisi Mkoani Kigoma limefanikiwa kuua majambazi watatu kati ya watano waliofanya tukio la unyanganyi wa kutumia silaha za jadi kwa kuteka gari aina ya Land Cruiser linalohudumia wakimbizi katika Kijiji cha Nyarulanga, Kata ya Busunzu, Wilayani Kibondo.

 

Akithibitisha kutokea tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoani Kigoma, ACP Martin Otieno amesema majambazi hao waliteka gari hilo linalomilikiwa na Shirika la Good Neighbour na kupora mali mbalimbali ikwemo laptop, simu na fedha ambapo thamani ya vitu vilivyoporwa ni zaidi ya laki tatu.

Toa comment