The House of Favourite Newspapers

Pombe yamuaibisha Mariah Carey

0

LAS VEGAS, NV - MAY 17:  Mariah Carey arrives at the 2015 Billboard Music Awards at MGM Garden Arena on May 17, 2015 in Las Vegas, Nevada.  (Photo by Steve Granitz/WireImage)

Las Vegas,  Marekani

Mwanamuziki Mariah Carey ambaye ni mama wa watoto wawili, Monroe na Moroccan juzikati alijikuta akiaibishwa na pombe ambazo alikunywa alipokuwa klabu jijini Las Vegas.

Awali, mwanamama huyo alionekana ameshika glasi ya pombe kisha akaanza kufanya vituko mbalimbali ikiwa ni pamoja na kumkumbatia DJ aliyekuwa akifanya mambo yake ukumbini hapo.

Mariah aliendelea kuchangamka na kuongea kwa sauti kubwa kupitia kipaza sauti pasipo mpangilio ambapo alikesha na kufanya vituko vingi ikiwa ni pamoja na kukisi na DJ huyo ambaye hana uhusiano naye.

Mbali na vituko hivyo, Mariah alionekana kuzidiwa mpaka kufikia hatua ya kuanguka na kujiachia nywele zake ambazo zilionekana kama za mwenda wazimu.

 Haijulikani ni kwa nini Mariah amefikia hatua ya kunywa pombe nyingi na kumuacha bilionea wake James Packer ambaye hutembea naye kila kona kwani kitendo cha yeye kunywa pombe si mara ya kwanza.

Leave A Reply