POSH QUEEN, PROF JAY GUMZO!

PICHA waliyopiga mwanamitindo Jacqueline Obed ‘Posh Queen’ na Mbunge wa Mikumi, Joseph Haule ‘Prof Jay’ imezua gumzo ile mbaya huko Instagram. Picha hiyo inayoaminika imepigwa hivi karibuni baada ya Posh kutembelea Bunge jijini Dodoma, imezua gumzo hilo kwa watu wengi kuhoji alikwenda kufanya nini mjini humo.

“Mh! Huyu Posh Queen kaenda kufanya nini jamani kama si** kwa kweli mjini mipango,” aliandika mdau mmoja mtandaoni huku wenzake wakimuunga mkono. Hata hivyo, kuna wengine walisema bungeni anaweza kwenda mtu yeyote hivyo isichukuliwe kama ni jambo la ajabu kwa mrembo huyo mwenye figa matata kutinga.

Loading...

Toa comment