POSH: SITUMII MWILI KUJIPATIA FEDHA

Queen Obed ‘Posh Queen’

MREMBO Queen Obed ‘Posh Queen’ amefunguka kuwa haamini kuutumia mwili wake kama biashara ili aweze kujipatia fedha kama ambavyo wanavyofanya warembo wengine kwa sababu hata Mungu hapendi. Akizungumza na Ijumaa, Posh alisema mwili na umbo zuri amepewa kama zawadi kutoka kwa Mungu hivyo hawezi kuutumia vibaya kwani atakuwa anamkosea aliyempa.

“Kuna watu wengi wananisumbua sana wakijua mimi ni kama wale, hapana, kiukweli ninajiheshimu na watu wanaonifikiria kuwa najiuza hivyo nawaambia kuwa hapa siyo mahali pake kabisa, nimeitafuta elimu ili niweze kupata kazi ya kujikimu maisha yangu mwenyewe,” alisema Posh.

Stori: Imelda Mtema, Dar

 

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO


Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Loading...

Toa comment