The House of Favourite Newspapers

Posho Nzito Simba Ikiiua Kaizer Chiefs

0

MTENDAJI Mkuu (CEO) wa Simba, Barbara Gonzalez ameweka bayana kwamba wanajua umuhimu wa mechi yao ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Kaizer Chiefs ambapo wamepanga kutoa bonasi nzito kwa nyota wa kikosi hicho.

 

Barbara ameongeza kuwa watakaa kikao na wachezaji wa timu hiyo kwa ajili ya kuwatangazia aina ya bonasi ambayo wataipambania kwenye mechi hiyo.

Simba, kesho Jumamosi watacheza na Kaizer Chiefs ukiwa mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika ambao utapigwa kwenye Uwanja wa FNB, Afrika Kusini.

 

Akizungumzia juu ya hilo, Barbara alisema: “Mambo yako vizuri na kila kitu kuhusu kikosi kipo vizuri, tuko tayari na morali iko juu.

 

Siku moja kabla ya mechi (leo Ijumaa) tutakaa nao na tutatangaza rasmi bonasi hili wakiwa uwanjani wajue wanapambana kwa ajili ya nini. Hii ni robo fainali tunajua tunachotaka.”

 

Mkwanja kwa mchezaji boraWakati huohuo, wachezaji wa Simba wamekewa mezani Sh milioni mbili kwa atakayefanikiwa kuibuka mchezaji bora wa mechi.

 

Taarifa ambazo Championi Ijumaa imezipata ni kuwa uongozi wa timu umepokea ofa ya zawadi ya Sh milioni mbili kwa mchezaji atakayefanikiwa kuibuka mchezaji bora wa mchezo huo iliyotolewa na wadhamini wa timu hiyo, Emirate Aluminum Profile.

 

“Kitu pekee ni kwamba wadhamini ndiyo wametoa bonasi kwa mchezaji ambaye atafanikiwa kuwa mchezaji bora wa mchezo na wao wamelenga kuongeza motisha ya wachezaji kujituma kwenye mchezo husika kwa kuwa timu inatafuta matokeo ya ushindi ili kuweza kusogea,” alisema mtoa taarifa.

Stori: Said Ally na Ibrahim Mussa

Leave A Reply