The House of Favourite Newspapers

POSHO YA OKWI, CHAMA INALIPA MSHAHARA YANGA

NEEMA imeendelea kuwashukia wachezaji wa Simba, unaambiwa kama mchezaji akicheza mechi ya Ligi Kuu Bara na timu ikapata ushindi, basi anapata posho ya shilingi 400, 000.

Kiasi hicho cha fedha kinapita baadhi ya waajiriwa wa Serikalini wakiwemo walimu na manesi ambao mishahara yao ya kila mwezi inakadiriwa kuanzia shilingi 300, 000.

 

Ukikusanya posho za mechi moja za Okwi na Claytous Chama zinaweza kulipa mshahara wa beki chipukizi wa Yanga, Paulo Godfrey ambaye juzi kwenye mechi dhidi ya Lipuli alilimwa kadi nyekundu. Simba hadi hivi tayari imecheza michezo kumi ya ligi huku ikashinda mechi saba, ikafungwa mchezo mmoja na Mbao FC na sare mbili dhidi ya watani wao Yanga, Ndanda FC.

 

Taarifa ambazo Spoti Xtra imezipata ni kwamba, posho hizo za 400,000 zinawahusu wale wachezaji wanaocheza mechi pekee na wanaokaa jukwaani wanaambulia uchakavu wa shilingi 80,000 pekee katika mchezo.

 

Mmoja wa vigogo wa Simba alisema wameweka kiwango hicho fedha kwa ajili ya kuongeza ushindani wa wachezaji ndani ya uwanja ili mmoja akipata nafasi ya kucheza, basi acheze kwa kiwango cha juu kwa mafanikio ya timu.

 

Alipotafutwa Mratibu wa timu hiyo kuzungumzia hilo, Abbas Ally alisema: “Posho kwa wachezaji zipo katika kuhakikisha morali ya wachezaji inaoongezeka ambayo ni siri nisingeweza kuiweka wazi.”

WILBERT MOLANDI, Dar es Salaam

WANACHAMA Simba Wapewa MashartI/ Uchaguzi Wapamba Moto

Comments are closed.