The House of Favourite Newspapers

Poshy Atamani Kukatiza Sokoni

MWANADADA mwenye shepu matata Bongo, Jacqueline Obeid ‘Poshy Queen’ ametoa kali ya mwaka, amesema anatamani kukatiza katikati ya soko kama alivyokuwa mtoto.

 

Akichonga na Shusha Pumzi, Poshy Queen alisema, anatamani mno kufanya mbishe hizo kama alivyofanya alipokuwa mdogo, lakini sasa hivi ni ngumu kutokana na shepu yake kwani baadhi ya wanaume wakware wamekuwa wakimsumbua kila anakokatiza kiasi cha kushindwa kutembea kawaida tu kwenda kununua matumizi ya nyumbani.

 

“Natamani sana kurudi utotoni, nilikuwa nakatiza popote kama sokoni kununua bidhaa bila usumbufu wowote, lakini sasa hivi nashindwa kwa sababu ya bugudha nyingi ila ipo siku nitatafuta ulinzi, nitaenda tu sokoni kununua ninachohitaji,” alisema Poshy.

STORI: IMELDA MTEMA

Comments are closed.