Poshy Queen Asherehekea Miezi Minne ya Mahusiano Mapya na Zawadi ya Gari

Poshy Queen, mrembo maarufu na sosholaiti kutoka Tanzania, amekuja tena kwenye vichwa vya habari baada ya kuweka wazi mahusiano yake mapya kupitia mtandao wa Insta baada ya kuachana na aliyekuwa mpenzi wake Mwimbaji maarufu wa Bongo Fleva, Rajab Abdul Kahali almaarufu Harmonize.
Hivi karibuni, aliweka picha ya Range Rover mpya aliyopokea kama zawadi kutoka kwa mpenzi wake, huku akielezea furaha yake kuhusu mahusiano yao.
Katika posti hiyo, Poshy Queen alisema:
“Nashindwa hata niseme nini.😩 sijui ulikuwa wapi siku zote daddy ❤️, lakini Mungu hachelewi wala hawai 🙌🏽🥰 Asante Mungu kwa kunipa the most intentional man 🙏🏽😘 siwezi kuelezea kila kitu but thank you for this byb wangu ❤️ hii ni miezi minne tukifika mwaka 🥲 🙌🏽😘❤️”
Kwa sasa, Poshy Queen anasema mahusiano yao yana miezi minne tu, lakini ana matumaini kuwa yatakuwa na mafanikio makubwa kadri yanavyokua, na anafurahi kuwa na mwanaume ambaye anampenda kwa dhati.