The House of Favourite Newspapers

Poshy: Wanawake Wanaongoza Kwa Chuki

0

Mrembo ambaye alijizolea umaarufu hivi karibuni baada umbo lake kuonekana kuwavutia watu mbalimbali bongo, Jacqueline Obeid ‘Poshy’ amesema alichojifunza kwenye dunia hii, wanaoongoza kwa chuki na roho mbaya ni wanawake na sio wanaume.

 

Akizungumza na Amani, Poshy, alisema kuwa amegundua kuwa kuna wanawake wengine hawapendi kuona mwingine anaendelea hivyo mwanamke huyo akiona mwenzake anapiga hatua, atamuwekea kila aina ya chokochoko ili kumtibulia mambo yake.

“Watu wanashindwa kuelewa kuwa huku duniani kila mtu ana bahati yake hivyo ukiona mwenzako anafanikiwa au mwanamke mwenzako anafanya vizuri mshike mkono uzidi kumfanya ainuke ili akuinue na wewe na sio kumponda kila kukicha maana huo utaitwa ni wivu,” alisema Poshy ambaye tayari amejikwamua kwa kufungua duka lake la kuuza nguo za ndani.

Stori: Imelda Mtema | IJUMAA

Leave A Reply