Post Malone Aweka Rekodi Kwenye Mauzo Ya Album Yake

 

MMWANAMUZIKI kutoka nchini Marekani, Post Malone amewka rekodi na album yake ya Hollywood’s Bleeding kwa kua ya kwanza kwa mwakanza 2019 kuuza nakala Zaidi ya Laki 1 kwa wiki nne tofauti za mwanzo.

Post Malone aliachia album hiyo Septemba 6 mwaka huu 2019 hivyo kuifanya kuwa album ya kwanza kwa zote zilizotoka mwaka huu kuuza nakala nyingi zaidi kwa wiki nne tofauti za mwanzo, mauzo yake hayajashuka chini ya nakala Laki 1.

Album hiyo ilivyotoka wiki ya kwanza iliuza nakala 489,000, Wiki ya pili iliuza nakala 198,000, Wiki ya Tatu iliuza nakala 149,000 na Wiki ya Nne imeuza Nakala 124,000.

Hollywood’s Bleeding ilikuwa album ya kwanza mwaka huu kukaa kileleni kwenye chart za ‘Billboard 200’ kwa wiki tatu mfululizo, Hata hivyo wiki hii imeshindwa kuonesha ubabe wake mbele ya album ya ‘KIRK’ ya DaBaby ambayo imeuza nakala 145,000.


Loading...

Toa comment