Poulsen amuongeza kiungo Yanga Stars

BENCHI la ufundi la Taifa Stars chini ya kocha wake, Kim Poulsen limemuongeza kiungo wa Yanga, Zawadi Mauya kwenye kikosi hicho kwa ajili ya kuchukua nafasi ya Mzamiru Yassin ambaye amekosekana kutokana na kuwa na kadi tatu za njano.

Wakati huohuo, nahodha wa Stars, Mbwana Samatta amesema kuwa Watanzania wasikate tamaa kwa sababu bado wanayo nafasi ya kufuzu Kombe la Dunia.

Samatta alisema wamefungwa nyumbani na Benin na wao wanaweza kushinda wakiwa ugenini na mbali na mechi hiyo bado watakuwa na mechi nyingine mbili mbele ambazo zinaweza zikawapa nafasi ya kuongoza kundi.

Stars waliodnoka nchini jana Ijumaa kuelekea Benin kwa ajili ya mchezo wa marudiano utakaopigwa kesho Jumapili.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Samatta alisema walichozidiwa na Benin ni maumbo ya wachezaji wao lakini kama kutengeneza nafasi wao walikuwa bora zaidi na mchezo ujao hawatarudia makosa.

“Watanzania wasiwe na mashaka na kukata tamaa juu ya timu yao, bado tuna nafasi kwenye kundi letu, wametuzidi pointi tatu, ambazo tunaweza kuzipata kwao, naamini hatutarudia makosa,” alisema Samatta.

ISSA LIPONDA, Dar es Salaam704
SWALI LA LEO

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?
Toa comment