The House of Favourite Newspapers

Poulsen: Cecafa U23 Itatuongezea Ufanisi Kuelekea Kombe la Dunia

0

KOCHA mkuu wa kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania, Kim Poulsen amefunguka kuwa ana matumaini makubwa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati (Cecafa), chini ya miaka 23, itawaongezea ufanisi zaidi wachezaji wake kuelekea kwenye maandalizi ya michezo ya kusaka tiketi ya Kombe la Dunia.

Ijumaa ya Julai 16, mwaka huu, Poulsen alitangaza kikosi cha wachezaji 20 wanaotarajiwa kuiwakilisha Tanzania katika michuano hiyo mikubwa kwa ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati.

Michuano hiyo kwa mwaka huu tayari imeanza rasmi kutimua vumbi jana Jumapili ambapo inafanyika nchini Ethiopia.

Akizungumza na Championi Jumatatu, kocha Poulsen alisema: “Tuna matumaini makubwa na vijana ambao tumewajumuisha katika kikosi chetu cha U23, hii ni kwa sababu kikosi hiki kina nyota wengi wenye vipaji na uzoefu mkubwa wa mashindano mbalimbali.

“Binafsi naamini tutafanya vizuri kwenye michuano hii, lakini pia tutaitumia kama sehemu ya maandalizi kuelekea kambi yetu ya mwezi Agosti ambayo tutaitumia kwa ajili ya maandalizi ya michezo yetu ya kusaka tiketi ya kushiriki michuano ya Kombe la Dunia.”

Leave A Reply