The House of Favourite Newspapers

POVU LA NAPE: “Kwa Hili… Serikali Imeisaliti Ilani ya CCM” – Video

Mbunge wa Jimbo la Mtama, Nape Nnauye, amesema kuwa wapiga kura wa mikoa ya Lindi na Mtwara walitegemea kupata neema kubwa kutokana na miradi ya gesi, na ndiyo jambo ambalo walilipa kipaumbele katika Ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwenye uchaguzi wa 2015.

 

Nape amesema kuwa ameshangaa kuona  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, hajalizungumzia kabisa suala hilo kwenye hotuba yake ya Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu aliyoiwasilisha bungeni wiki iliyopita .

 

“Nilipoangalia kwenye hotuba ya Waziri Mkuu, kuanzia ukurasa wa mwisho sikuona hata neno gesi, inaonekana shughuli za gesi zimesimama au zimeanza kufungwa Lindi na Mtwara. Naona jitihada kubwa inaelekezwa kwenye Mradi wa Stieglers Gorge na tumeuacha umeme wa gesi.

 

“Lakini tukumbuke Stieglers haimo kwenye Ilani ya CCM.  Tukumbuke ndani ya Ilani tumezungumzia nishati ya gesi, upo mpango wa LNG Plant, na hii ndiyo ilikuwa imani ya wana-Lindi na Mtwara. kuna watu walikufa kwa sababu ya gesi Lindi na Mtwara, walipoteza mali na wengine ni vilema.

 

“Kama ndiyo hivyo, je hatusaliti ilani ya CCM? Hatuwasaliti wana-Lindi na Mtwara waliotupa kura na kutuamini kwamba gesi yao iko salama? Hili ni bomu kubwa. Wawekezaji wameanza kuondoka, hali imekuwa ngumu. Namuomba Waziri Mkuu hili suala la gesi lisimfie mikononi mwake,” amesema Nape.

 

VIDEO: POVU LA NAPE SIKIA MWENYEWE

Comments are closed.