Premier kuomboleza kupotea kwa Sala
UONGOZI wa Ligi Kuu ya England ‘The Premier League’ umethibitisha kuwa timu zote shiriki zitakuwa na dakika moja ya ukimya kwa ajili ya kumbukumbu ya tukio la kupotea mchezaji Emiliano Sala aliyekuwa amesajiliwa na Cardiff City.
Sala alipotea akiwa pamoja na rubani David Ibbotson ambapo walikuwa safarini kutoka Ufaransa kuelekea Wales kujiunga na timu hiyo ambayo ilimsajili kwa pauni milioni 15.
Hatua hiyo imekuja baada ya uthibitisho kuwa Sala alikuwemo katika ndege hiyo ambayo ilipotea Jumatatu wakiwa hewani wakitokea Nantes. Premier League imethibitisha kuwa inafanya hivyo kuungana na wadau wa soka na familia ya wahusika hao.
Sala alikuwa ametoka kuwaaga wenzake wa Nantes kwa ajili ya kwenda kuanza maisha mapya katika Klabu ya Cardiff. Kumekuwa na taarifa kuwa uwezekano mdogo wa kuwapata wahusika hao waliopotea kwa kuwa haijulikani wako wapi na hakuna dalili za kuonyesha kuwa wako hai.
Comments are closed.