The House of Favourite Newspapers

Pretty Kind: Sina Ukimwi, nimeamua tu kuokoka

Msanii wa muziki na filamu Bongo, Suzan Michael ‘Pretty Kind’

KUTOKANA na tetesi kuzagaa kwamba ameathirika na ugonjwa wa Ukimwi, ndiyo maana ameamua kuokoka, msanii wa muziki na filamu Bongo, Suzan Michael ‘Pretty Kind’ ameibuka na kufungukia tuhuma hizo.

Akizungumza na Mikito Nusunusu, Pretty Kind alisema amekuwa akisikia habari hizo kuwa ana Ukimwi, jambo ambalo siyo kweli hivyo ameamua kumkabidhi Mungu maisha yake na siyo vinginevyo.


“Nimeamua kubadilika tu, maisha ya wokovu ni mazuri zaidi kuliko ya duniani, nimeokoka na ninasali kwenye kanisa la kilokole linaloitwa Rhema The Faithful Church, yaani kwenye kanisa hili ni sehemu ambayo Mungu amenibadilisha.

“Wanaosema nimeathirika na Ukimwi wanakosea, siyo kila anayeokoka ana Ukimwi jamani, nimebadili mfumo wa maisha yangu na maisha ndani ya Yesu nayafurahia sana,” alisema Pretty ambaye alifungiwa kufanya sanaa kwa miezi sita kabla ya kufunguliwa.

STORI: Mikito Nusunusu

Comments are closed.