The House of Favourite Newspapers

Prezzo: Tungepata Marais 10 Kama JPM Tungekuwa Mbali

KWA mara ya kwanza tangu aingie kwenye muziki, rapa kutoka Kenya, Jackson Ngechu Makini ‘Prezzo’ ameshindwa kuzuia hisia zake baada ya kuweka wazi kuwa anamkubali sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli na kwamba Afrika ingepata marais 10 kama yeye basi ingefika mbali sana.

 

Prezzo aliweka picha katika ukurasa wake wa Instagram ikimuonesha Rais Magufuli akimsaidia mama mmoja ambaye alishindwa kulipa pesa alizokuwa anadaiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kuandika;

 

“Hii ilini-touch (ilimgusa), Afrika tungekuwa na viongozi kumi kama Mheshimiwa Magufuli (Rais Magufuli) kwa kweli tungekuwa mbali sana badala ya kupata taabu saaaana. Mwenyezi Mungu azidi kubariki kazi ya mikono yako Your Excellency.”

 

Baada ya kuweka posti hiyo, ndani ya muda mfupi mashabiki walitoa maoni yao kuhusu video hiyo iliyopostiwa na Prezzo ambapo waliandika;

 

“Iliumiza wengi sana, tuna Rais mwenye huruma sana hasa kwa wanyonge.” @Eunice 8181.

“Bonge la point bro. dingi huyu ni mashine na hana uoga kabisa, hata wazungu anawachana live bila kupepesa macho.” John Maniha.

 

“President Magufuli Mungu azidi kumlinda na pia ampe maisha mazuri more life Mr president your humanity is a gift from God.” Asiimwe David.

 

Ikumbukwe Prezzo ameingia rasmi kwenye siasa baada ya kutangazwa kugombea Ubunge katika Kaunti ya Kibra iliyopo Kusini mwa Jiji la Nairobi, msanii mwingine ambaye ameingia katika siasa ni Jose Chameleone kutoka nchini Uganda.

 

Kama watafanikiwa kushinda katika chaguzi zao wataungana na wasanii ambao wapo kwenye uongozi wa siasa kama Prof. Jay , Joseph Mbilinyi “Mr II Sugu”, na Jaguar kutoka Kenya.

Comments are closed.