Priyanka Chopra Anatamani Kuwa Mama

 

MWIGIZAJI maarufu duniani kutokea nchini India Priyanka Chopra amekiri kuchoshwa na maisha ya kuhamahama na anatamani pia yuko tayari kuwa mama.

Priyanka Chopra aliiambia Press trust of India, kuwa kwasasa anahitaji sana kutulia na mume wake Nick Jones na anataka kupata uzoefu wa kuwa mama.

“Nimekuwa nikiishi maisha ya kawaida sana, ila kwasasa ningependa kutulia na kupata mtoto, nimeshoot filamu nyingi mno zilizonigharimu kuhamahama ila sasa ntayaweka pembeni ilikutimiza ndoto yangu”

Priyanka Chopra 37′ mwigizaji anaelipwa mtonyo mrefu zaidi nchini India na Nick Jones 27 mwanamuziki kutoka Marekani, walifungandoa Dec mwakajana. Na kutokaa mahala pamoja kwa takriban miez 9 kutokana na kutingwa kwa Priya kwenye kuigiza.


Loading...

Toa comment