Producer wa Kimataifa Aliyefanya Kazi na Whozu, Mabantu Kaachia Dude

MSANII maarufu nchini SWITZERLAND, Fame Luck ameachia albamu yake mpya hivi karibuni iitwayo Here I Am ambayo imkuwa ikifanya vizuri kwenye mitandao mbalimbali na platform za muziki duniani.

Fame Luck ambaye pia ni Producer mkubwa na wa kimataifa, ameitendea haki labamu yake hiyo ambayo nyimbo zake zimekuwa zikigongwa kwenye kumbi mbalimbali za starehe, sherehe na maeneo ya bata.

Msanii huyo ni miuongoni mwa maproducer wachache duniani ambao wana uwezo wa kufanya production ya muziki wakati huo huo, wakaimba na ngoma na zikahiti

Staa huyo ambaye kipaji chake kingine kikubwa ni DJ wa ukumbini, amekuwa gumzo katika maeneo mbalimbali duniani ikiwemo Bongo kwani tayari ameshafanya kazi na wasanii wa hapa Tanzania kama Whozu, kundi la Mabantu na wengine.

Zaidi kabisa ni kwamba, Fame anamiliki Studio zake zinazoitwa Marrakech Music, na tayari ameshawasaidia wasanii, maproducer na MaDjs kibao kutusua katika tasnia ya muziki kimataifa.

Baadhi ya wasanii wengine wakubwa kimataifa ambao Fame amefanya nao kazi na kuwasaidia kutoboa international ni Diplo, Skrillex, Major Lazer, Avicii, DJ Snake na wengine kibao.

Nyimbo zilizomo ndani ya albamu yake ya Here I Am ni; You Give Me Life, Give It to Me, Why Did I Let You Go, Here I Am, I See a Picture, Mamacita, Taboo, Through the Pain, Hold You Down, Strong na Codx.

Tazama ngoma zake hapa ==> FAME LUCK

 

Toa comment