Profesa Jay Aachia Siku 462 Kuelezea Mateso Aliyoyapata Tangu Aanze Kuumwa
Siku 462 ndiyo habari ya mjini! Huu ni wimbo mpya wa @professorjaytz ambao ameuachia rasmi leo, Novemba 6, 2023 akielezea safari yake ya ugonjwa, kuanzia siku ya kwanza mpaka alipokuja kuruhusiwa hospitali, akiwa amekaa siku 462.
Tayari wimbo huo unapatikana mjini Youtube, kwenye akaunti yake inayokwenda kwa jina la Profesa Jay, akiwa amemshirikisha Walter Chilambo.
Nenda kausikilize!