Msanii mkongwe wa Hip Hop na Mb8nge wa Chadema Jimbo la Mikumi, Joseph Haule ‘ Profesa Jay’ (kulia) akiwa na Mhariri msadizi wa Gazeti la Amani, Andrew Carols jana baada ya kufanya mahojiano na Global TV Online.
Mhariri wa Risasi Jumamosi, Erick Evarist akiwa na Profesa Jay (kulia).
Mhariri wa Championi Ijumaa, John Joseph (kushoto) akiwa katika pozi na Jay.
Mhariri Kiongozi wa Championi, Saleh Ally (kulia) akifanya yake na Profesa.
Walusanga Ndaki akisalimiana na Profesa Jay.
Edwin F Linde (kushoto) akifanya yake na Profesa Jay.
Mtunzi wa Hadithi Global, Ally Mbetu akimpongeza Profesa Jay kwa kazi yake mpya ya Kazi Kazi.
Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Global, Clarence Mulisa akiwa na Jay.
Wafanyakazi wa Global wakiwa katika pozi mbalimbali na Profesa Jay.
Jay, anayechukuliwa kama ndiye aliyeshawishi umma kuukubali muziki wa kizazi kipya kutokana na mashairi yake ya kuelimisha, anasema alipofika bungeni baada ya kuchaguliwa kuwa mbunge wa Mikumi, alipokelewa na viongozi wote kwa kumhimiza kutoacha muziki, kwani ana kipaji nao.
Jay, alisema siku zote amekuwa ni mtu wa kuwapa nguvu watu waliokata tamaa, akisema yeyote anaweza kuwa yeyote.
Kuhusu kususia kwao vikao vya bunge, Jay ambaye ni mbunge kupitia Chadema inayounda Ukawa, alisema wanafanya hivyo kwa sababu ndiyo njia pekee ya kutuma ujumbe kuwa hawaridhiki na kufungwa kwao mdomo, kwani hicho ndiyo amekuwa akikipigania siku zote.
“Mimi ni Voice of speechless yaani Sauti ya wasiosikika, kwa hiyo kama tunafungwa midomo tusiseme tulichotumwa na wapiga kura wetu siyo sawa, tumekatazwa kufanya mikutano, sasa leo mimi nimewapigania wapiga kura wangu na nimepewa fedha za maji, nitafanyaje kuwaeleza kilichotokea? Tunasusia vikao ili kupeleka ujumbe kuwa haturidhiki na kinachotokea bungeni, bunge linatakiwa kuisimamia serikali, lakini kilichopo ni serikali kulisimamia bunge.”