The House of Favourite Newspapers

Profesa Jay: Mimi nilikuwa mbunge kabla sijaingia bungeni

0

Professor Jay ndani ya Global (1)Msanii mkongwe wa Hip Hop na Mb8nge wa Chadema Jimbo la Mikumi, Joseph Haule ‘ Profesa Jay’ (kulia)  akiwa na Mhariri msadizi wa Gazeti la Amani, Andrew Carols jana baada ya kufanya mahojiano na Global TV Online.

Professor Jay ndani ya Global (2)

Mhariri wa Risasi Jumamosi, Erick Evarist akiwa na Profesa Jay (kulia).

Professor Jay ndani ya Global (8)

Mhariri wa Championi Ijumaa, John Joseph (kushoto) akiwa katika pozi na Jay.

Professor Jay ndani ya Global (16)

Mhariri Kiongozi wa Championi, Saleh Ally (kulia) akifanya yake na Profesa.

Professor Jay ndani ya Global (3)

Walusanga Ndaki akisalimiana na Profesa Jay.

Professor Jay ndani ya Global (5)

Edwin F Linde (kushoto) akifanya yake na Profesa Jay.

Professor Jay ndani ya Global (6)

Mtunzi wa Hadithi  Global, Ally Mbetu akimpongeza Profesa Jay kwa kazi yake mpya ya Kazi Kazi.

Professor Jay ndani ya Global (7)

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Global, Clarence Mulisa akiwa na Jay.
Professor Jay ndani ya Global (9) Professor Jay ndani ya Global (10) Professor Jay ndani ya Global (11)Wafanyakazi wa Global wakiwa katika pozi mbalimbali na Profesa Jay.

MSANII mkongwe wa Hip Hop, Joseph Haule maarufu kama Profesa Jay jana alitinga katika studio za Global Tv Online na kufanya mahojiano yaliyogusa maeneo mbalimbali.
Jay, anayechukuliwa kama ndiye aliyeshawishi umma kuukubali muziki wa kizazi kipya kutokana na mashairi yake ya kuelimisha, anasema alipofika bungeni baada ya kuchaguliwa kuwa mbunge wa Mikumi, alipokelewa na viongozi wote kwa kumhimiza kutoacha muziki, kwani ana kipaji nao.
“Mimi nilikuwa mbunge kabla sijaingia bungeni kwa sababu siku zote nyimbo zangu zilikuwa ni zenye kuelimisha, kutia moyo na kukosoa pale panapostahili, kule viongozi wengi waliniambia nisiache muziki na mimi siwezi kuacha, lakini hivi sasa nimepewa jukumu na watu wa Mikumi, la kuwa mtetezi wao pale mjengoni, kwa hiyo nitakuwa mbali kidogo na mashabiki, lakini siwezi kuwaacha kabisa, ndiyo maana nimewadondoshea hii ngoma mpya ya Kazi Kazi.”
Jay, alisema siku zote amekuwa ni mtu wa kuwapa nguvu watu waliokata tamaa, akisema yeyote anaweza kuwa yeyote.
“Ndiyo maana kichupa (video) ya wimbo huu nilienda kushutia kule Uwanja wa Fisi, kwa watu wa chini. Mimi nafahamu maisha yetu yote yalivyo magumu, lakini nimeweza kupambana na leo ni Mbunge, ndoto zangu ni kuwa Rais, kwa hiyo hata wao wanaweza kusimama katika ndoto zao na kufikia malengo bila kujali wako wapi kwa sasa,” alisema.
Kuhusu kususia kwao vikao vya bunge, Jay ambaye ni mbunge kupitia Chadema inayounda Ukawa, alisema wanafanya hivyo kwa sababu ndiyo njia pekee ya kutuma ujumbe kuwa hawaridhiki na kufungwa kwao mdomo, kwani hicho ndiyo amekuwa akikipigania siku zote.

“Mimi ni Voice of speechless yaani Sauti ya wasiosikika, kwa hiyo kama tunafungwa midomo tusiseme tulichotumwa na wapiga kura wetu siyo sawa, tumekatazwa kufanya mikutano, sasa leo mimi nimewapigania wapiga kura wangu na nimepewa fedha za maji, nitafanyaje kuwaeleza kilichotokea? Tunasusia vikao ili kupeleka ujumbe kuwa haturidhiki na kinachotokea bungeni, bunge linatakiwa kuisimamia serikali, lakini kilichopo ni serikali kulisimamia bunge.”

(Habari na Abraham Ojukwu/GPL)
Leave A Reply