Professa Awapa Mtihani Wanafunzi Kutafuta Marafiki 1,667, Ili Kufaulu

 

PROFESA mmoja katika chuo cha uchumi na sheria nchini  China ametoa mtihani kwa wanafunzi wa chuo hicho wa kutafuta marafiki 1667 kupitia mtandao wa WeChat ambao ni mtandao maarufu sana wa kijamii nchini humo.

 

Jaribio hilo litabeba maksi 60 kati ya 100 kwenye somo hilo.   Kwa jinsi marafiki watakavyokuwa wakiongezeka ndivyo mwanafunzi atajipatia nafasi ya maksi kuongezeka mpaka kufikia A+ endapo atafikisha marafiki 1667.

Baadhi ya wanafunzi chuoni hapo wamelalamika kwamba kazi hiyo ni ngumu, lakini imeonekana kwamba itawasaidia katika maisha yao ya baadaye.

 

“Ni vigumu kazi hii kukamilika, ninao marafiki 100 tu kwenye WeChart,wengi wetu tunajisikia huzuni na woga kwamba hatutaweza kukamilisha jambo hili,”.alisema mwanafunzi mmoja

 

Zoezi hilo limetolewa kwa muda wa siku 10 ambapo inampasa kila mwanafunzi kulikamilisha ili kufikisha maksi 60.

Loading...

Toa comment