PROMOSHENI MAGAZETI YA GLOBAL YATIKISA KIBAMBA MPAKA KIBAHA

Wasomaji wa kituo cha bodaboda cha Mbezi Luguruni wakiwa makini kufuatilia magazeti ya Risasi na Championi.

Promosheni ya Magazeti ya Global Publishers leo Jumatano, Novemba 7, 2018 imeendelea kuchanja mbuga ambapo ilikuwa ni pande za Kibamba, Kiluvya mpaka Kibaha ambapo wasomaji wa magazeti kawa kawaida walionekana kugombea magazeti yaliyokuwa yakinadiwa leo ambayo ni Risasi Mchanganyiko na Championi ambayo hutoka kila Jumatano.

Vijana wachapakazi wa Kiluvya Madukani, Kijiwe cha Mti Pesa wakiwa makini kusoma magazeti la Global.

Wasomaji waliopata nafasi ya kutoa maoni yao katika magazeti hayo walisema wanapendezwa zaidi mambo mbalimbali yaliyomo katika magazeti hayo zikiwemo habari motomoto, hadithi za kusisimua, katuni, burudani na mambo mengine mengi.

Matukio katika Picha: 

Ofisa Usambazaji wa Global, Mussa Mgema (wa pili kushoto) akiwaelekeza jambo Mama Lishe wa Njia Panda ya Mloganzila baada ya kujipatia gazeti la Risasi.

Wakazi wa maeneo hayo walionekana kuvutiwa na magazeti ya Risasi na Championi na wengi wao wakayachangamkia kwa kuyanunua magazeti hayo ambayo yana habari za uhakika na zenye manufaa makubwa kwa jamii.

Ofisa Usambazaji wa Global, Charles Mponzi (kushoto) akiwaelekeza jambo wasomaji wa Mbezi Luguruni.

Magazeti haya ya Championi na Risasi Mchanganyiko yanapatikana mtaani kila Jumatano ya wiki kwa bei ya Tsh. 800 tu!

Wasomaji wa Kibamba Shule wakifuatilia gazeti la Championi.  

Fundi cherehani wa Kibamba CCM akisoma gazeti la Risasi wakati akiwasubiri wateja wafuate nguo zao na wengine wampelekee kazi.

Mtaalamu wa kupika chapati, Kibamba Njia Panda ya Mloganzila, Jasmin Mrangi, akiwa na tabasamu wakati akisoma gazeti la Championi.

Mwananchi wa Kiluvya Madukani akijisomea gazeti la Championi.

 

HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS / GPL           

 

Toa comment