The House of Favourite Newspapers

Promosheni Ndogo za Shinda Nyumba Kufanyika Mtaa kwa Mtaa

0
Afisa Masoko wa Global wakiendelea kuwaelekeza wananchi namna ya kujaza kuponi.

WAKATI droo ndogo ya tatu ya Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba Awamu ya Pili ikibakia kuwa historia, mhamasishaji mkuu wa promosheni hiyo maarufu kwa jina la Mr. Shinda Nyumba, mwanzoni mwa wiki hii alikuwa kivutio katika mitaa ya Kigogo-Luhanga jijini Dar.

Akiwa na ‘kruu’ nzima ya promosheni hiyo katika mitaa mbalimbali ya Kigogo, wananchi wengi walionekana kuvutiwa naye, hasa kwa urefu wake na kujumuika naye ambapo aliwaeleza umuhimu wa kushiriki bahati nasibu hiyo ya aina yake.

Mr Shinda nyumba akiendelea kugawa zawadi mitaani.

“Ni mara chache kukutana na bahati kama hizi, hiyo mia tano yako ambayo unainunulia vitumbua inaweza kukupatia pikipiki, simu ya kisasa, dinner set, tivii kubwa na zaidi inaweza kukupa hata nyumba, hebu jaribu leo kununua magazeti ya Global Publishers, uone unavyoweza kushuhudia maajabu,” alisema Mr. Shinda Nyumba aliyelazimika kupozi kila wakati ili kupiga picha na wasomaji waliokuwa wamemzunguka.

Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho alisema kampuni inaendelea kuboresha zawadi kwa washindi wa droo ndogo kwa kadiri inavyowezekana ili kuhakikisha watu wanabadili maisha yao kupitia bahati nasibu hiyo ambayo hivi sasa ni gumzo. Alisema baada ya hapo awali kutoa zawadi ya simu aina ya Tecno, hivi sasa zimeboreshwa zaidi kwani zinatolewa Smartphones za aina mbalimbali ambazo ni za kisasa.

“Tupo katika uboreshaji wa zawadi hizi wakati tukiendelea na droo ndogo zitakazofuata, kwa hiyo wasomaji waendelee kusoma magazeti yetu  na kukata kuponi kwa ajili ya kushiriki bahati nasibu hiyo, huenda wakafanikiwa kubadili maisha yao,” alisema.

Naye Yohana Mkanda, ambaye ni Afisa Masoko wa Global Publishers, aliwahimiza wasomaji kuendelea kusoma magazeti ya Ijumaa, Uwazi, Championi, Risasi, Amani na Ijumaa Wikienda, kwani kadiri wanavyokata kuponi zao, nafasi ya ushindi inazidi kuwa karibu yao.

“Kama mnavyojua, hii ni bahati nasibu, lolote linaweza kutokea, hawapaswi kudharau kwa sababu shilingi mia tano tu inaweza kubadili maisha yako, ni rahisi sana kushiriki mchezo huu.

“Katika magazeti yetu yote, kwenye kurasa za pili zipo kuponi zenye maelekezo ya namna ya kufanya, ukishamaliza kujaza, wanaweza kuzituma kwetu kupitia kwa mawakala wetu waliopo nchi nzima na wale wa Dar es Salaam wanaweza kuja ofisini kwetu, Bamaga Mwenge na kuziacha kwenye ndoo ya kukusanyia kuponi,” alisema Mkanda. Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba Awamu ya Pili imedhaminiwa na Kampuni ya Tecno Mobile, King’amuzi cha Ting, British School na Kilimanjaro Institute of Technology.

Leave A Reply