The House of Favourite Newspapers

Watoto Yatima Na Wanaoishi Kwenye Mazingira Magumu Mkoani Rukwa Wakumbukwa

0
Msamaria Mwema na mkazi wa mkoani Rukwa, Prudencia Paul Kimiti akiwa amewabeba watoto hao alipowatembelea.

Msamaria Mwema na mkazi wa mkoani Rukwa, Prudencia Paul Kimiti ametembelea na  kukabidhi msaada wa vitu mbalimbali katika vituo vya kulelea  watoto yatima vya Peter’s House Bangwe na Katandala Orphanage Center vilivyopo mkoani Rukwa.

Kituo cha kwanza alichotembelea ni kituo cha Peter’s House kilichopo Kata ya Izia mtaa wa Bangwe ambapo katika kituo hicho, Prudencia alitoa vifaa vya shule kwa wanafunzi ambao wanasoma shule mbalimbali za serikali na binafsi wanaosomeshwa na kituo hicho.

Amekabidhi madaftari ya kuandikia na Ma counter books ya kumtosha kila mwanafunzi, kalamu za wino, kalamu za risasi na mikebe na alitoa pia aliwapa juice, mchele na kuacha pesa za kununulia nyama ili watoto waweze kula na kufurahi kwa pamoja kama watoto wengine wanaoishi kwa wazazi wao.

Kituo cha pili alichotembelea ni kituo cha watoto yatima cha Katandala yaani Katandala Orphanage Centre kinachopatikana Kata ya Katandala ambapo katika kituo hicho Prudencia alitoa msaada wa maziwa kwa watoto wachanga, mkaa wa kupikia na kuacha pesa ya kulipia bili ya umeme.

Prudenciana akiwa na baadhi ya watoto hao.

Aidha, alifarijika sana kuona wanafunzi wote wanaosoma katika vituo vyote viwili kuwa na uwezo mkubwa wa kitaaluma katika masomo yao, na alipowahoji baadhi yao walimueleza kuwa wanasoma kwa bidii ili waweze kuwa madaktari na wengine Wanajeshi ili kuisaidia nchi na watu wake hapo baadae.

Hata hivyo, Prudencia anatoa rai kwa wadau wa ustawi na maendeleo jamii mkoa wa Rukwa kuendelea kushirikiana na vituo hivi ambavyo vinalea watoto waliobeba ndoto za kuisaidia nchi siku za usoni.

Pia, anawapongeza TRA Sumbawanga kwa kuwa karibu kusaidia mahitaji muhimu ya mara kwa mara katika kituo cha Peter’s House.

Leave A Reply