PSPF wapeleka huduma mpya ya Bima ya Afya Majira, Mwananchi

1Mkurugenzi wa Mipango naUwekezajiwa PSPF, Bw. Gabriel Silayo (wanne kushoto) akisisitiza jambo katika kikao kazi kilichowakutanisha watendaji wakuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF na Business Times. Menejimenti ya PSPF ipo katika ziara ya kutembelea vyombo vya habari kwa lengo la kutolea ufafanuzi juu ya masuala mbalimbali ya Mfuko na kutambulisha huduma mpya ya Bima yaAfya.2Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu akifafanua jambo kwa Wahariri wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) alipotembelea Makao Makuu ya MCL, TabataRelini jijini Dar es salaam, kulia ni watendajiwa PSPF.3Meneja Mkuu wa Business Times Limited Bw. Aga Mbuguni (kushoto) akipokea machapisho mbalimbali ya Mfuko wa Pensheni wa PSPF kutoka kwa Mkurugenzi mkuu wa Mfuko huo Bw. Adam Mayingu baada ya kikao cha watendaji wakuu wa taasisi hizo kilichofanyika Makao Makuu ya Business Times jijini Dar es Salaam.4Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd, Bw. Francis Nanai (kushoto) akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugezi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, baada ya kikao kazi kati ya Wahariri wa Mwananchi na Watendaji wa PSPF, kushoto ni Bw. Daniel Mwaijega Meneja Utawala Idara ya Habari na kulia ni Bibi. Matlida Nyalu Afisa wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari wa PSPF.

Mkurugenzi Mkuu wa PSPF Bw. Adam Mayingu aliongoza ujumbe wa watendaji wakuu wa PSPF kutembelea vyumba vya habari vya magazeti ya Mwananchi na Majira, ikiwa ni utaratibu wa PSPF wa kutembelea vyombo vya habari kwa lengo la kufahamiana, kutolea ufafanuzi masuala mbalimbali na kupokea ushauri wa kuboresha huduma za PSPF.

Katika ziara hiyo iliyofanyika Desemba 2, 2015, Mkurugenzi wa PSPF aliongozana na Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji, Bw. Gabrilel Silayo, Mkurugenzi wa Uendeshaji, Bibi Neema Muro, Mkurugenzi wa TEHAMA, Bw. Andrew Mkangaa, Meneja wa Mawasiliano, Masoko na Uenezi, Bibi. Costantina Martin, Afisa kutoka Mpango wa Uchangiaji wa Hiari wa PSPF, Bibi. Mathilda Nyallu na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF Bw. Abdul Njaidi.

Kituo cha kwanza cha safari hiyo ilikuwa katika ofisi za gazeti la Majira wachapishaji wa Gazeti la Majira na Business Times ambapo walikutana na watendaji wakuu wa kampuni hiyo.

Pia viongozi hao wa PSPF walitembelea ofisi za Mwananchi Communications zilizopo Tabata, ambapo walikutana na watendaji wakuu wa gazeti hilo. Katika maeneo yote watendaji wa PSPF walijibu maswali mbalimbali, walipokea ushauri na kutambulisha huduma ya Bima ya Afya inayotolewa na PSPF kwa kushirikiana na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.

“Lengo la ziara hizo ni kuwatembelea wenzetu wa vyombo vya habari kwa lengo la kufahamiana, kutolea ufafanuzi juu ya masuala mbalimbali ya PSPF na kujifunza kutoka kwao jinsi ya kuboresha huduma zetu, pia kwa sasa tunatangaza huduma yetu mpya ya Bima ya Afya,hivyo tupo katika mpango wa kuwaelimisha waandishi wa habari ili na wao waweze kuelimisha umma juu ya mpango huo ambao ni mkombozi kwa watanzania wengi…huu ni mwendelezo kwani tulianza ziara hizi tangu mwaka jana,” alifafanua Bw. Mayingu.

Loading...

Toa comment