The House of Favourite Newspapers

PSPF Yavuna Wanachama VOWET

0

????????????????????????????????????Meneja wa Mfuko wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari (PSS), wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Mwanjaa Sembe, (aliyesimama), akiwaongoza wanachama wapya waliojiunga na mpango huo, wakati wa warsha ya siku moja iliyowakutanisha maafisa na mabalozi wa PSPF, na wanakikundi wa Sauti ya Wanawake Wajasiriamali Tanzania, (VOWET), kwenye ukumbi wa Belmonte jijini Dar es Salaam, Oktoba 13, 2015.

????????????????????????????????????

Balozi wa PSPF, Mwanamitindo wa Kimataifa aishie nchini Marekani, Flaviana Matata

????????????????????????????????????

????????????????????????????????????

Magire Werema, Afisa Masoko Mwandamizi wa PSPF

????????????????????????????????????

????????????????????????????????????

????????????????????????????????????

Balozi wa PSPF, Msanii maarufu Tanzania, Mrisho Mpoto akitoa mada

????????????????????????????????????

Mwanachama wa VOWET, akijaza fomu tayari kuwa Mwanachama wa PSPF, kupitia mpango wa PSS

????????????????????????????????????

Wanachama wapya wakijaza fomu.

????????????????????????????????????

Afisa Masoko Mwandamizi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Rahma J Ngassa, (kushoto), akiteta jambo wa Balozi wa Mfuko huo, Flaviana Matata.

????????????????????????????????????

????????????????????????????????????Meneja wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari (PSS), wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Mwanjaa Sembe, akitoa mada.

????????????????????????????????????Meneja wa Mpango wa PS, Mwanjaa Sembe, (kushoto), akimsikiliza Mjumbe wa Bodi ya VOWET, Anne Ottieno wakati akijiandaa kujaza fomu za kujiunga na Mpango huo.

????????????????????????????????????

Mjumbe wa Bodi ya Sauti ya Wanawake Wajasiriamali Tanzania, VOWET, Anne A. Ottieno, akiuliza swali.

NA K-VIS MEDIA

MFUKO wa Pensheni wa PSPF, umezidi k”kupenya’ kwenye sekta binafsi na kuvuna wanachama zaidi kupitia mpango wake wa uchangiaji wa hiari yaani PSS, ambapo wanakikundi wajasiriamali wa kundi la Sauti ya Wanawake Wajasiriamali Tanzania (Voice of Women Entrepreneurs Tanzania-VOWET).

Wanachama hao wapya walijiunga baada ya kushiriki warsha ya siku moja ambayo ilifanyika kwenye ukumbi wa Belmonte ulioko jingo la makao makuu ya PSPF, jijini Dar es Salaam Oktoba 13, 2015, ambapo Mabalozi wa Mfuko huo, Msanii wa majigambo, Mrisho Mpoto na Mwanamitindo wa Kimataifa anayeishi na kufanyia kazi zake jijini New York Marekani, Flaviana Matata, walishiriki kutoa “Darasa” kuhusu umuhimu wa Watanzania walio katika sekta bionafsi kuchangamkia fursa kupitia kuiunga na uamancaha wa Mfuko huo kupitia mpango wa PSS.

Mabalozi hao waliongozwa na Meneja wa Mpango wa PSS, Mwanjaa Sembe, na Afisa Masoko Mwandamizi wa Mfuko huo, Magire Werema, ambao wote kwa pamoja walifafanua na kueleza kwa kina faida za kuwa mwanachama wa Mfuko huo, ambapo kwa muda mfupi baada ya kujiunga Mwanachama anawezakufaidi mafao mbalimbali yatolewayo na Mfuko huo ikiwemo mikopo ya nyumba, Fao la Elimu, na mengine mengi.

Kufuatia :Darasa” hilo, wanachama wa VOWET walijiunga na Mfuko huo kupitia mpango wa PSS

(Picha na K-VIS MEDIA/Khalfan Said)

Leave A Reply