The House of Favourite Newspapers

PSSSF Yatwaa Tuzo ya Umahiri Katika Uwasilishaji Taarifa za Mahesabu Kwa Mwaka 2021

0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Jamal Kassim Ali (Kushoto) akimkabidhi tuzo ya Umahiri katika uandaaji na uwasilishaji taarifa za fedha kwa mwaka 2021, Mkurugenzi wa Fedha Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Beatrice Musa-Lupi wakati wa kilele cha miaka 50 ya Boadi ya Wahasibu na Wakaguzi wa Maheabu Tanzania (NBAA) .

 

 

MFUKO wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umetwaa Tuzo ya Umahiri katika Uwasilishaji  wa Taarifa za Mahesabu kwa mwaka 2021, kundi la Mifuko ya ifadhi ya Jamii na Bima ya Afya.

 

Tuzo hiyo inayotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) imepokelewa na Mkurugenzi wa Fedha, PSSSF, Bi. Beatrice Musa-Lupi katika hafla iliyofanyika katika hotel ya APC Bunju jijini Dar es Salaam Novemba 30, 2022 ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, CPA. Jamal Kassim Ali.

 

PSSSF imetwaa tuzo hiyo ya umahiri katika uandaaji wa Taarifa za Fedha ya Mwaka 2021 (Best Presented Financial Statements for the Year 2021 Awards) kwa mwaka wa pili mfululizo.

Akizungumza kufuatia ushindi huo, Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF CPA. Hosea Kashimba alisema , tuzo hiyo itaongeza chachu kwa watumishi wa PSSSF katika kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia weledi na hivyo kuendelea kutoa huduma bora kwa wanachama wa Mfuko.

 

Aidha Mkurugenzi wa Fedha, PSSSF, Bi. Beatrice Musa-Lupi alisema  ushindi huo ni ishara ya kwamba PSSSF inaandaa mahesabu kwa kuzingatia vigezo vilivyowekwa kimataifa lakini pia inaashiria uwepo wa weledi wa tasnia husika kwa upande wa watumishi.

 

“Sambamba na hayo niliyoyasema pia inaashiria uwepo wa usimamizi makini wa fedha za wanchama na hii inatupatia  heshima kama taasisi.” Alisema Mkurugenzi huyo wa Fedha PSSSF.

 

Aliwahakikishia Wanachama  dhamira ya PSSSF ya kuhakikisha usalama wa michango yao unazingatiwa kwa kiwango cha juu wakati wote, ikiwa ni pamoja na kuwepo uwazi kwenye usimamizi na utunzaji wa rasilimali za Mfuko.

“Ushindi huu pia unaashiria uwepo wa kesho ya wanachama wetu kama kaulimbiu yetu inavyosema   Leo. Kesho. Pamoja.” Alihitimiaha Bi. Beatrice Musa-Lupi.

 

Naye mgeni rasmi katika hafla hiyo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Ikulu, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, CPA. Jamal Kassim Ali amewaagiza wahasibu na wakaguzi wa hesabu nchini kufanya kazi kwa kuendana na ukuajiwa Sayansi na Teknolojia ili kuharakisha utoaji wa taarifa za mahesabu kwa umma.

b

Pia amewasihi wahasibu na wakaguzi wa hesabu kufanya kazi kwa uadilifu na kuzingatia miiko na maadili ya kazi yao kwani taaluma hiyo ni muhimu katika uchumi wan chi na ustawi wa maendeleo.

 

 

Amewapongeza wote walioshinda tuzo za umahiri katika uandaaji na uwasilishaji wa taarifa za mahesabu kwa mwaka 2021.

Leave A Reply