Puma Yachangia Mitungi ya Gesi Katika Shughuli za Mbio za Mwenge Chalinze

Puma Energy Tanzania inaendelea kushirikiana na serikali katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia ambapo imeshiriki katika hafla ya Mbio za Mwenge wa Uhuru katika Wilaya ya Chalinze zilizofanyika jana mkoani Pwani.
Mkuu wa Kitengo wa Gesi ya PumaGas Bw. Jeffrey Nasser alikabidhi mitungi ya gesi kwa Mkuu wa Wilaya ya Chalinze Mhe. Shaibu Issa Ndemanga na Kiongozi Mkuu wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2025 ndugu Ismail Ali Ussi.

Hii ni dhamira ya kampuni ya kuendelea kuhakikisha jamii inakua salama na safi kwa kutumia nishati safi ya kupikia.
