The House of Favourite Newspapers

Putin Amuondoa Sergei Shoigu kama Waziri wa Ulinzi wa Urusi

0

Rais wa Urusi Vladimir Putin amemuondoa mshirika wake wa muda mrefu Sergei Shoigu kama waziri wa ulinzi katika mabadiliko aliyoyafanya katika Baraza lake la mawaziri,Kremlin imetangaza.

Shoigu mwenye umri wa miaka 68 amehudumu katika wadhifa huo tangu 2012.

Nyaraka zilizochapishwa na baraza la juu la bunge la Urusi zilisema nafasi ya Shoigu itachukuliwa na Naibu Waziri Mkuu Andrei Belousov.

Shoigu amekuwa na mchango mkubwa katika vita vya Urusi na Ukraine.

Nyaraka hizo za serikali ya Urusi zinaonyesha Putin anataka Bw Shoigu achukue nafasi ya Nikolai Patrushev katika baraza la usalama lenye nguvu.

Bado haijabainika Patrushev utapewa wadhifa gani katika mabadiliko hayo.

Shoigu ana uhusiano wa karibu na Rais Putin, mara nyingi humpeleka katika safari za uvuvi katika nchi yake ya asili ya Siberia.

Alipewa nafasi ya ulinzi licha ya kutokuwa na historia ya kijeshi katika hatua ambayo iliwakera baadhi ya ya wakuu wa jeshi wa ngazi ya juu.

Shoigu alipata umaarufu kama mkuu wa wizara ya dharura na misaada ya majanga katika miaka ya 1990.

Leave A Reply