The House of Favourite Newspapers

PWEZA WA KUKAANGA

NI Jumamosi nyingine tena mpenzi msomaji tunakutana na leo tutaangalia pishi la pweza wa kukaanga kama wengi wenu mlivyoomba.

MAHITAJI

-Pweza kilo moja.

-Mafuta nusu kikombe.

-Chumvi kijiko kimoja cha chai.

-Tangawizi mbichi iliyosagwa kijiko kimoja cha chai.

-Vitunguu saumu vilivyosagwa kijiko kimoja cha chai.

-Masala kijiko kimoja cha supu.

KUTAYARISHA NA KUPIKA

-Chukua pweza mkatekate vipande unavyotaka.

-Osha na maji safi na salama.

-Weka viungo vyote kwenye pweza pamoja na chumvi .

Acha kwa nusu saa ili akolee viungo.

Weka ndani ya sufuria bila maji mfunike kisha weka jikoni, atatoa maji mwenyewe kwa moto wa kiasi mpaka awe na rangi ya kahawia. Akishaiva kwa rangi hiyo basi mwaga maji yote, chukua pweza pekee weka kwenye bakuli au sahani. Bandika kikaango kwenye moto, weka mafuta, acha kwa muda wa dakika tano hivi ili yapate moto kisha mimina pweza kwenye kikaango, acha wakaangike mpaka wabadilike rangi huku ukiwageuzageuza kila baada ya muda wa dakika kumi. Baada ya hapo pweza wako atakuwa tayari kwa kuliwa kwa ugali au muhogo.

Comments are closed.