The House of Favourite Newspapers

Q Chilla Afunguka Alivyotoweka kwa Siku 3

MARA baada ya kuzua hofu kwa familia pamoja na watu wake wa karibu, staa wa muziki wa Bongo Fleva, Abou-bakar Katwila ‘Q Chilla’ ameibuka na kueleza alivyotoweka kwa siku tatu.

Hivi karibuni, msanii huyo alitoweka katika mazingira ya kutatanisha huku akizua hofu kwa familia yake, watu wake wa karibu pamoja na mashabiki kuwa huenda ametekwa ama kufanyiwa vitendo vya kikatili.

 

Akizungumza na Risasi Vibes, Q Chillah aliwaomba radhi mashabiki, familia na watu wake wa karibu wote walioguswa baada ya kutoonekana kwake huku akitaja sababu kuwa ni mawasiliano.

“Nimeumia sana, sikujua kama haya mambo yatakuwa makubwa kiasi hiki. Kuna rafiki yangu mmoja alinifuata hapa Dar na kuniambia kuwa ana mazungumzo maalum na mimi.

 

“Sikumkatalia, tukapanga kwenda kuyafanyia mkoani Morogoro, tukaenda huko hadi sehemu moja inaitwa Matombo. Kufika nikaona kuna view nzuri ambayo naweza kuja kutengeneza video siku za mbeleni, basi tukazidi kusonga kumbe sikujua huku nyuma mawasiliano yanakata. Simu yangu ikakata netiweki na tayari tulikuwa mbali sana,” alisema Q Chillah.

 

Q Chillah aliongeza kuwa, ilimchukua siku mbili kuwepo huko Matombo.

“Siku ya tatu narudi, simu yangu bado ikawa inasumbua netiweki, nikashug-hulikia na kukutana na meseji na simu nyingi kutoka kwa familia, ndugu, marafiki na mashabiki wangu.”

Comments are closed.