The House of Favourite Newspapers

Q Chilla Apaa Kimataifa na Patoranking

q-chief-42-of-248

MKALI wa Muziki wa Bongo Fleva, Abubakar Katwila ‘Q Chillah’ baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu ameibuka kwa kishindo kizito kwa kufanya kolabo na msanii wa Nigeria, Patoraking.

Kupitia Global TV Online, Q Chillah amesema wimbo huo kwa mara ya kwanza atautambulisha rasmi katika Uwanja wa Samora mkoani Iringa.

“Nilikuwa kimya sana ila kwa sasa nimerudi upya, mtazamo wangu ni wa kimataifa zaidi na nimefanikiwa kufanya wimbo na Patoranking ambao nitautambulisha rasmi Desemba 5, mwaka huu, mkoani Singida,” alisema Q Chillah.

Q Chillah aliongeza kuwa, wimbo huo umefanywa na watayarishaji watatu akiwemo, Abidady na D. Touch kutoka Tanzania na Suka Rekodi ya Nigeria chini ya Kampuni ya QS Mhonda Entertainment.

Na Gabriel Ng’osha

Comments are closed.