The House of Favourite Newspapers

Q Chillah: Gharama za Video Zangu Unajenga Nyumba -Video

MSANII nguli katika ‘Industry’ ya Bongofleva, Abubakar Shaban Katwila,almaarufu kama Q Chillah, leo Augosti 2, 2019 amefanya mahojiano maalumu na + 255 Global Radio katika kipindi cha Bongo255.

Q Chillah ambaye ‘ameshikwa mkono’ na Harmonize siku za hivi karibuni kwa ajili ya kumrudisha kwenye sanaa ya muziki, mbali na kuja kutambulisha nyimbo zake mpya alizotoa ambazo ni My Boo (Remix), Nionyeshe na Go Low ambazo zote ameshirikiana na msanii Harmonize, pia amezungumzia maisha yake, alivyoyumba kimuziki na changamoto alizopitia yeye na familia yake baada ya anguko lake la kimuziki.

” Watoto wangu wamesoma kwa manyanyaso sana kwa sababu ya mapito ya mimi baba yao. Lakini nashukuru mungu nimepata nafasi nyingine na ninajua wapi nilikosea.”

Akizungumzia  gharama ya video zake zilizotoka hivi karibuni, Q Chillah amesema video hizo zimegharimu pesa nyingi ambazo ni zaidi ya Sh. milioni 40, gharama ambayo yote ametoa msanii Harmonize. Akaongeza kuwa Harmonize ni mdogo kiumri, lakini anamuongoza kwenye mambo mengi  kisanaa na amemhakikishia kuwa baada ya miezi michache ataanza kupiga shoo za zaidi ya Sh. milioni 20.

Alipoulizwa kuhusu kumsaidia Chid Benz aachane na matumizi ya madawa, Q Chillah amesema: ”Chid Benz ni msanii mkali sana kwa hapa Afrika Mashariki, nampenda sana. Anahitaji msaada wa ziada kurudi kwenye mstari sahihi, nikiweza nitamsaidia,”

Pia Q Chillah  amempa ushauri huohuo msanii mwenzie, TID,  kuwa aachane na tabia aliyonayo, na arudi kwenye tasnia.

Comments are closed.