The House of Favourite Newspapers

Q CHILLAH NI SHULE YA BURE KWA CHID BENZ

Tokeo la picha la Q CHILLAH
Abubakar Shabaan Katwila ‘Q Chillah’

NILIPOKUWA kijana mdogo, nikiishi kwenye mitaa wa uswahilini Kirumba mwanzoni mwa miaka ya 2000, mwanamuziki Abubakar Shabaan Katwila ‘Q Chillah’ alikuwa kila kitu kwangu. Niligeza nyimbo zake, nilivaa kama yeye, nilitengeneza nywele zangu kama yeye, nilitembea kama yeye, kiufupi sikuhitaji kufananishwa naye tu, bali nilihitaji kuwa kama yeye mwenyewe. Wimbo wake wa Si Ulinikataa ulikuwa unanikumbusha namna baba yangu alivyoukataa ujauzito wangu na kusababisha mama yangu alee ujauzito kwa shida na tabu hata akanizalia mitaani. Wimbo wa Ninachokipata ndiyo huwa unaniliza kabisa.

Unanikumbusha machungu ya maisha ya mitaani na namna mama yangu alivyokufa baada ya kubakwa na kuambukizwa virusi vya Ukimwi, pamoja na hayo wimbo wake wa Dreamer kiukweli huwa unanifuta machozi na kunifanya niamini kwamba maisha hayamaanishi machungu tu niliyopitia, lakini kuna ‘future’ mbele ambayo inaweza kunifuta machozi.

Wengi wanaweza kufikiri hii ni simulizi ya kweli, lakini ukweli ni kwamba si halisi. Nimejaribu kutengeneza picha na kukuonyesha maisha ya baadhi ya wasanii yanavyowagusa watu, watu wanavyoyaishi na namna nyimbo zao zinavyomaanisha kwenye maisha yao. Sasa jiulize mtu kama huyu aliye ndani ya maisha ya Q Chillah aliposikia jamaa ametopea kwenye matumizi ya dawa za kulevya alikuwa ‘dissapointed’ kiasi gani! Hakika ni zaidi ya fikra za kawaida.

Hata hivyo, leo nina habari njema kwa mtu huyu na Watanzania wote. Nimefanya mahojiano na Q Chillah, hakika si yule tena ambaye alikuwa anasemwa vibaya kwa matumizi ya dawa za kulevya, ananyimwa sapoti kwenye media na kutia huruma.Tokeo la picha la Q CHILLAH

Q Chillah amebadilika kuanzia maisha yake, mtazamo wake, namna ya kuendesha muziki wake na mengine mengi. Kwa mabadiliko haya hakika amekuwa shule ya bure kwa wanamuziki wengine wengi wakiwemo Chid Benz aliyejiingiza kwenye matumizi ya dawa za kulevya. Ungana naye kwenye mahojiano haya na Showbiz Xtra!

Showbiz: Hongera kwa ujio wako mpya wa Kisamvu?

Chillah: Asante sana. Mapokeo ni makubwa ndani na nje ya Bongo, kiukweli ni ‘fire’, nawashukuru Watanzania kwa sapoti yao.

Showbiz: Nini hatuki-fahamu nyuma ya ujio huu?

Chillah: Ujio huu ulikamilika takribani miezi miwili iliyopita, lakini menejimenti yangu haikuniruhusu niutoe kwanza. Nilitakiwa kuzungumza kwanza na watu wa saikolojia wanielekeze baadhi ya vitu na ushauri kwenye masuala mbalimbali ikiwemo kutunza na kukuza kipato changu.

Showbiz: Lakini umewashangaza wengi, ulitangaza kuacha muziki ila umetoa ujio mpya, ulikuwa unatafuta kiki au kipi kimetokea?

Chillah: Haikuwa kiki. Nilikuwa siriazi na wengi wenu mnafahamu mambo ambayo yanaendelea kwenye muziki. Wingi wa siasa na sitaki kuzama huko. Siku nilipomaliza mahojiano nilipigiwa simu na mtu kutoka Marekani akaniambia nitengue kauli yangu.

Alinishangaza, lakini baada ya kufanya mazungumzo akaniambia anahitaji kunisimamia. Kwa hiyo hapo ndipo nilipopata tumaini jipya na kwa menejimenti hii kiukweli nipo kwenye mikono salama. Inaitwa Alfa Chain International, masikani yake ni Marekani, ina matawi Sauz, Rwanda na hapa Bongo.

Showbiz: Inasemekana pia JPM (Rais John Magufuli) ana mkono wake kukubakiza kwenye muziki?

Chillah: Ni kweli nilipotangaza kuacha muziki, alituma wawakilishi wake tuweze kuzungumza kabla ya kutokomea moja kwa moja nje ya gemu.

Showbiz: Mlizungumza nini?

Chillah: Siwezi kuweka wazi kila kitu. Bado tupo kwenye mazungumzo kwa hiyo baadaye ukifika wakati wa kuyaweka wazi mazungumzo yetu, nitayaweka wazi.

Showbiz: Naona pia umekuwa balozi wa umoja wa mataifa, ni balozi wa nini na ilikuwaje mpaka ukapata nafasi hiyo?

Chillah: Mimi ni balozi wa watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu. Nilipata nafasi hiyo baada ya kujitolea kuhudhuria mara kwa mara kwenye semina zao. Nimekwenda mkoani Simiyu baadaye Rwanda na sehemu nyingine. Kwa hiyo nimeonekana ninafaa ndiyo maana nimepewa hii nafasi.

Showbiz: Kiukweli unaon-ekana umeba-dilika. Nini hasa siri ya kubadilika kwako?

Chillah: Nimebadilika kwa sababu niliamini hakuna wa kunibadilisha zaidi ya mimi mwenyewe. Sikuhitaji kwenda soba, wala kutegemea watu kunib-adilisha.

Ninach-oweza kusema baada ya kugundua kwamba nimekosea, nilijipa moyo nakubadilisha baadhi ya vitu vilivyokuwa vinanipoteza. ‘Life style’, marafiki na mengine mengi. Lakini pia nilifahamu kwamba nipo kwenye daraja muhimu kwenye maisha yangu ambalo lilinihitaji nivuke kwenda kule ninakotakiwa kuwa. Ndipo hapa nilipo sasa.

Showbiz: Hongera sana Chillah. Jambo la mwisho kwa Watan-zania kama unalo.

Chillah: Wanipe sapoti na kunipokea Q Chillah mpya kama ilivyokuwa siku zote.

Comments are closed.