The House of Favourite Newspapers

QNET Kuleta bidhaa zake za kuboresha maisha nchini Tanzania

Meneja wa QNET, kanda kusini ya Afrika Biram Fall (katikati) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa maonesho ya bidhaa za QNET 2019 jijini Dar Es Salaam jana. Wengine kwenye picha ni Mkuu wa Elimu ya Mtandaoni wa QNET Bernie Gaksh (kushoto) na Mshauri wa Biashara wa QNET Tanzania, Edward Mkony.

 

Kampuni yenye asili ya Asia ya mauzo ya moja kwa moja QNET itaendesha maonyesho ya bidhaa na huduma zake jijini Dar es salaam siku ya tarehe 16 na 17 Machi 2019 katika ukumbi wa Mlimani City kuanzia saa 4 asubuhi mpaka saa 1 Jioni.

 

Maonyesho yenye jina la Absolute Living, (Kuishi Kikamilifu) sambamba na falsafa ya bidhaa za kampuni ya mauzo ya moja kwa moja, huwa yanafanyika kila mwaka katika nchi mbalimbali duniani kote ikiwa na lengo la kuonyesha bidhaa zake na huduma kwenye masoko mapya. Onyesho hilo pia linakuwa kama jukwaa kwa wateja na wadau wengine wanaotaka kufahamu kuhusu QNET na mtindo wake wa biashara.

 

Nadharia ya Absolute Living (Kuishi Kikamilifu) inaakisi juhudi za QNET za kukuza mwenendo wa kujali afya, mtindo wa maisha wenye uwiano sahihi, ikiwa inatilia mkazo katika Afya, Ustawi na Elimu.

Akizungumza kwenye mkutano na vyombo vya habari Meneja Mkuu wa Kanda wa QNET kwa Kanda ya Kusini mwa Jangwa la Sahara Afrika, Biram Fall alisema kwamba, "Tunatoa aina mbalimbali za bidhaa za kiwango cha juu na huduma kwa wateja wetu kuwasaidia waweze kuishi maisha yenye uwiano sahihi, na pia kutatua tatizo la msingi kama vile elimu, ufahamu, na maendeleo binafsi kupitia program za mafunzo yetu, ambayo yanawasaidia katika safari yao ya kujiajiri mwenyewe.

 

 

Kutoka katika kozi za elimu kwa njia ya mtandao kama vile SELI/qLearn, mpaka katika vifurushi vya sikukuu kama vile Tripsavr, mpaka bidhaa za kuongeza nguvu kama vile Bio Disc3, virutubisho kama EDGE, na saa za mkononi kama Bernhard H. Mayer, QNET ina aina mbalimbali za kukidhi mahitaji mbalimbali ya watu. Katika kitovu cha yote haya, ni hamu yetu ya kutoa fursa ya Kuishi Kikamilifu "Absolute Living” Zaidi ya watu elfu mbili wanatarajiwa kuhudhuria maonyesho ya siku 2 ambayo yatakuwa na bidhaa za mfano katika onyesho, na kuonyesha namna ya matumizi ya bidhaa na faida zake kwa wateja na watumizji wa mwisho. Kwa kuongezea, wataalamu wa bidhaa na biashara watakuwepo kwa ajili ya kujibu swali lolote kutoka kwa wageni ili kuelewa vizuri ulimwengu wa QNET.

 

QNET inaalika watu wote kuhudhuria onyesho hili jijini Dar es salaam na kujifunza kwanza kuhusu bidhaa, huduma na fursa za biashara. Maonyesho ya Dar es salaam yanafuata mfululizo wa maonyesho kama hayo yaliyofanikiwa nchini Togo, Guinea, Ivory Coast, Senegali, Burkina Faso na Cameroon mwaka jana.

 

Msafara wa maonyesho utasisimama katika mji wa Kumasi, Ghana, baada ya Dar es salaam kuanzia
tarehe 23 mpaka 24 Machi mwaka 2019. Mwisho// Kuhusu QNET QNET ni moja kati ya makampuni ya mauzo ya moja kwa moja kutoka Asia yanayoongoza ambayo inatoa aina mbalimbali za bidhaa za afya, ustawi na mitindo ya maisha ambayo yanasaidia watu kuishi maisha bora zaidi. Kwa miaka 20, Mtindo wa biashara ya kuanzia
ngazi ya chini ya QNET umeongezewa kasi na nguvu ya biashara ya mtandao imesaidia kuwawezesha mamiloni ya wajasiriamali katika nchi zaidi ya 100 duniani kote.

 

Makao makuu ya QNET yako Hong Kong na imefungua ofisi zake katika zaidi ya nchi 25 duniani kote kupitia kampuni tanzu, ofisi za matawi yake, ushirikishaji wa mawakala na uwakala. QNET ni mwanachama wa Chama cha wauzaji wa moja kwa moja (Direct Selling Association) cha Malayasia, Singapore, Ufilipino, Indonesia na UAE, pamoja na Chama cha Chakula Bora cha Hong Kong (Hong Kong Health Food Association) na Chama cha
viwanda vya Virutubisho vya afya cha Singapore (Health Supplements Industry Association)
miongoni wa vingine.

 

QNET pia inafanya vizuri katika udhamini wa michezo duniani. Baadhi ya ushirikiano wakubwa inajumisha kuwa mshirika wa mauzo wa moja kwa moja wa Klabu ya Mpira wa miguu ya Manchester City Football Club na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kwajili ya Ligi ya Mabingwa ya Total ya CAF, Kombe la Shirikisho la Total CAF na Kombe la Total CAF Super Cup kwa mwaka 2018 na 2019. Kwa taarifa zaidi, tafadhali tembelea tovuti ya QNET kupitia www.qnet.net

Comments are closed.