QUEEN DARLEEN AFUNGUKIA NGUO ZA MITEGO

 

Queen Darleen’

MSANII wa Bongo Fleva ambaye ni dada wa mwa­namuziki mkubwa wa Afro-Pop, Na­sibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Mwana­hawa Ab­dul ‘Queen Darleen’ amefun­guka kuwa nguo anazovaa za kimitego zinazoacha sehemu kubwa ya mwili wake hazina madhara kwake na kwa mpen­zi wake.  Darleen aliliambia Risasi Jumamosi kuwa, mara nyingi anaona watu wanamse­ma kuhusu nguo anazovaa, lakini hawajui kwamba yeye kama mwanamuz­iki ndizo nguo anazo­paswa kuvaa.

“Kinach­onishangaza ukivaa kibukta, utasikia watu wanakusema umekaa uchi, sasa sijui wa­nataka nikiwa ninapanda stejini nivae khanga? Maana hata huyo mpenzi wangu haongei chochote kuhusu mavazi yangu jamani,” alisema Darleen.

STORI: Imelda Mtema, Dar

Toa comment