Queen Darleen amfanyia kufuru Mbosso

DADA wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Mwanahawa Abdul ‘Queen Darleen’ hivi karibuni alimfanyia kufuru msanii mwenzake, Yusuf Mbwana Kilungi ‘Mbosso’ kwa kummwagia minoti kama yote.

 

Tukio hilo lilitokea Jumatano iliyopita nyumbani kwa Mbosso, Sinza-Lion, Dar kulikokuwa na sherehe ya mwanaye aliyezaa na mpenzi wake, Rukia Rucky ya kutimiza siku 40 tangu kuzaliwa ambapo ulipofika wakati wa kutoa zawadi, Queen Darleen alimwaga fedha ambazo kwa kukadiria ni zaidi ya shilingi laki tano.

rleen

Kutokana na kumwaga fedha huko, Queen Darleen aliwaacha watu midomo wazi huku wakijiuliza ni wapi anapata jeuri hiyo ya fedha kwa sababu kwenye muziki hayuko vizuri kama zamani.

“Huyu ni mwanamuziki mwenzangu na ni mwana

familia kwenye Lebo ya Wasafi Classic Baby ‘WCB’ hivyo lazima nimpe zawadi ili afurahi aone kama tuko pamoja,” alisikika akisema Queen Darleen alipokuwa akimwaga fedha.

Toa comment