Queen Darleen Amshangaa Hamorapa…

Queen Darleen

Na ALLY KATAMBULA| GAZETI LA UWAZI| SHOWBIZ

MWANAMUZIKI anayefanya vizuri kwenye tasnia ya Muziki wa Bongo Fleva akiwa chini ya Lebo ya WCB,  ‘Queen Darleen’  hivi karibuni ameonyesha kushangazwa na kitendo cha mwanamuziki chipukizi Hamorapa kujifananisha na Hermonize.

Hamorapa

Akipiga stori na Uwazi Showbiz, hivi karibuni na kutakiwa kuzungumzia kauli aliyoitoa Dancer Mose Iyobo ambaye yupo kwenye Lebo ya WCB kuwa Hamorapa anafanana na sokwe alisema hamjui msanii huyo kivile na anamshangaa kujifananisha na Harmonize.

“Hata kama nilishamuona sijamtilia maanani, simjui kabisa na sidhani kama anafanana na Harmonize, lakini  pia siwezi kuzungumzia lolote juu ya kauli ya Iyobo,” alisema Queen Darleen

Toa comment