Queen Darleen Amwaga Machozi Msiba wa Dansa wa Alikiba – Video

MSANII wa Bongo Fleva kutoka Lebo ya WCB, Queen Darleen amejikuta akimwaga machozi baada ya kuona hali ya afya ya aliyekuwa Dansa wa Msanii Alikiba, Emma 4 Real aliyeaga dunia majuzi na kuzikwa jana jijini Dar es Salaam.

 

Akizungumza na Global TV Online kwenye msiba huo, shangazi wa Emma alisema moja ya wasanii walioguswa na ugonjwa wa Emma ni Queen Darleen ambaye ni Dada wa Diamond Platnumz, baada ya kusikia alichukua usafiri na kumfuata mgonjwa hadi hospitali kumjulia hali, lakini alipoona hali ya afya ya dansa huyo, alimwaga machozi.

 

“Siku ambayo Emma alizidiwa tulichukua bajaji tukampeleka hospitali, wakati dereva wa bajaji akirudi alikutana na Queen Darleen na kumweleza kuhusu hali ya mgonjwa, aliamua kuchukua usafiri na kwenda hadi hospitali, yeye alikuwa akidhani kwamba huenda anaumwa malaria ya kawaida, lakini alipomuona hali yake, alimwaga machozi palepale,” amesema Shangazi.

 

FUATILIA MAHOJIANO HAYO HAPA

Toa comment