Queen Darleen Ataja Siri ya Ushindi wa Zuchu

STAA wa muziki wa Bongo Fleva na memba wa Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB), Mwanahawa Abdul ‘Queen Darleen’, afunguka kuhusu Zuchu.

Akizungumza na Risasi, Queen Darleen amesema kuwa Zuchu ni msanii ambaye walihakikisha wanamtengeneza na kupata kile anachokihitaji.

“Zuchu ni msanii ambaye tulimtengenezea mazingira, anatakiwa kujiheshimu. Tulijaribu kumchunga na kumtunza kwa sababu alikuwa akihitaji vitu vyote hivyo,’’ alisema Darleen ambaye ni First Lady wa WCB.

STORI: HAPPYNESS MASUNGA

Toa comment