QUEEN DARLEEN: MAMA YANGU KAFUNGWA CHINA?

Mwanahawa Abdul ‘Queen Darleen’

MSHANGAO! First Lady wa Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB), Mwanahawa Abdul ‘Queen Darleen’ ameshtushwa na tetesi za mama yake mzazi kuwa amefungwa nchini China kwa msala wa madawa ya kulevya. 

 

Awali zilienea stori mitandaoni kuwa mama wa msanii huyo alidakwa miaka mingi nchini humo na kufungwa jela.

Akizungumza na Over Ze Weekend juu ya ishu hiyo, Darleeen aliweka wazi kuwa, aliposikia hata yeye alishtuka na kwamba ni uvumi tu kwani mama’ke yupo hapa nchini na hapendi mambo ya mitandao.

 

“Mama yangu kafungwa China? Niliposikia nilishangaa sana kwani mama yangu yupo na mtu akitaka anione nimpeleke nyumbani,” alisema Queen Darleen ambaye ni dada wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz

STORI: SHAMUMA AWADHI, DAR

Toa comment