Queen Darleen: Mke wa Poli Naye Mke

FIRST Lady wa Wasafi Classic Baby (WCB), Mwanahawa Abdul ‘Queen Darleen’ amefunguka kuwa haoni tatizo kuolewa mke wa pili na wanaomsema wala hana habari nao!

 

Akizungumza na Risasi Vibes, Darleen amesema kuwa yeye ameolewa kabisa kwa taratibu kamili za Kiislamu, sasa ni mke halali, hajampora mtu, ameolewa kama wanawake wengine.

 

“Unajua watu hawaelewi, mke wa pili wanamweka sijui kwenye kundi gani maana mimi ni mke halali kama alivyooa Mtume wake wanne, alikosea kwani jamani? Dini yetu inaruhusu kabisa,” alisema Queen.

Stori: IMELDA MTEMA

 

Toa comment